Kitabu cha maelekezo kwa mafundi au opereta kuhusu uboreshaji wa usalama, afya na mazingira ya kazi katika sekta isiyo rasmi

Kitabu hiki kina maelekezo yanayoonyesha jinsi ya kufanya mabadiliko yaliyorahisi, yene ufanisi na gharama nafuu katika sekta isiyo rasmi, ambayo yataboresha usalama, afya na mazingira ya kazi na hatimae kuongeza tija.

Instructional material | 01 March 1999
Njia hii ya uboreshaji wa usalama, afya na mazingira ya kazi imetokana na mafunzo ya majiribio, uzoefu wa kazi wa muda mrefu na uchambuzi nakini wa mahitaji ya mafundi au opereta waliopo katika sekta isiyo rasmi. Mafunzo yaliopo katika njia hii yamelenga katika kuwahamasisha waajiri na opereta wao kufanya mabadiliko ya dhati palepale wanapofanyia kazi. Yaliyomo ni pamoja na mawazo na ushauri unaofaa kuhusiana na maswala kama vile vumbi, chemikali, uzuiaji moto, ukaaji wakati wa kufanya kazi mbali mbali, maeneo ya kazi, huduma ya kwanza na kadhalika. Kitabu kinazungumzia maswala ya muhimu kwa usalma na afya kazini.

Msisitizo wa maelekezo yaliyomo umezingatia uwezekano, unafuu wa gharama na matumizi ya njia au vitu vinavyoweza kupatikana katika mazingira yetu ili kuboresha namna ya utendaji kazi na mazingira yake. Kila kipindi cha mafunzo lazima kizingatie kujenga uzoefu utakaoweza kuigwa katika mazingira ya kazi yaliyopo na jinsi ya kutambua namna ya kuboresha eneo la kazi la mshiriki.

Utekelezaji wa njia hii ya mafunzo umetokana na uzoefu uliopatikana toka nchi za Afrika na hasa Tanzania, na upo katika misingi ya uzoefu halisi wa mafundi au opereta wa sekta isyo rasmi ambao wameshiriki katika mradi wa mafunzo wa majaribio uliokuwa chini ya usimamizi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Zana za kufundishia njia hii kwanza ziliandaliwa wakati wa Mradi wa Ushirikiano wa Idara mbali mbali za Sekta Isiyo Rasmi Mijini yaani Interdepartmental Project on Urban Informal Sector of the ILO, mwaka wa 1995-96. Baadae zana hizo zilijaribiwa na kuhakikiwa katika Miradi mbali mbali ya Ushirikano wa kitaalamu.

Mashirika ya ILO/UNDP kupitia Mradi wake wa Uongezaji wa Ajira Mijini uliofanyika Tanzania mwaka 1998, yamewezesha kupatikana kwa mchango mkubwa wa jitihada za kufanikisha mafunzo kwa njia hii.